Luneng,China.
MSHAMBULIAJI wa Italia,Graziano Pelle,ameihama Southampton na kujiunga na klabu ya Shandong
Luneng inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini China kwa Mkataba wa Miaka Miwili na Nusu kwa dau la Paundi Milioni 13.
Pelle,30,atavuna Mshahara wa Paundi Milioni 34 kwa Kipindi cha Miaka Miwili na Nusu atakachokuwa akiitumikia Miamba hiyo ya Luneng.
Pelle aliyekuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Southampton anakuwa mchezaji wa pili kutoka Ligi Kuu ya England kujiunga na Shandong Luneng baada ya Juzi Jumamosi mshambuliaji wa Senegal,Papis Cisse aliyejiunga na klabu hiyo kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
0 comments:
Post a Comment