Liverpool,England.
KIPA wa zamani wa Arsenal na Austria,Alex Manninger,ameanza kujinoa na Liverpool ili kuangalia uwezekano wa kupata nafasi ya kusajiliwa kwa kandarasi ya mwaka mmoja klabuni hapo.
Manninger mwenye umri wa miaka 39 ameanza kujifua na Liverpool wiki hii baada ya kutemwa na iliyokuwa klabu yake ya awali ya Augsburg inayoshiriki ligi ya Bundesliga.
Kwa mujibu wa Tony Barrett,wa gazeti la The Times ni kwamba Kipa huyo Mkongwe ametua Liverpool baada ya kupata Mwaliko toka kwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Mjerumani,Jurgen Klopp.
Manninger aliwahi kuichezea Arsenal kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2002.Katika kipindi hicho chote alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 30 pekee ya Ligi Kuu England.Baadae alijiunga na Juventus ya Italia.
Ikiwa Manninger atafanya vizuri Liverpool itamsajili na kumfanya Kipa chaguo LA tatu nyuma ya Simon Mignolet na Loris Karius.
0 comments:
Post a Comment