728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 08, 2016

    MWINGEREZA ATEULIWA KUCHEZESHA FAINALI YA EURO 2016

    Saint-Denis,Ufaransa.

    SHIRIKISHO la vyama vya soka Barani Ulaya (UEFA) limemteua mwamuzi wa Uingereza,Mark Clattenburg,kuchezesha mchezo wa Fainali wa kuwania Ubingwa wa Euro 2016 utakaochezwa Jumapili Julai 10 huko Saint-Denis kati ya wenyeji wa michuano hiyo Ufaransa na Ureno.

    Uteuzi huo unamfanya,Clattenburg,41,kuwa na msimu mzuri katika kazi yake ya uwamuzi kwani mwaka huu tayari alishapewa dhamana ya kuchezesha Fainali ya kombe la FA Cup na ile ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.

    Katika michuano ya Euro inayoendelea tayari,Clattenburg,ameshachezesha jumla ya michezo minne mpaka sasa.Michezo hiyo ni ile ya Italia dhidi ya Ubelgiji,Croatia dhidi ya Jamhuri ya Czech, Iceland dhidi ya Austria, mchezo za mwisho ni ule wa Switzerland dhidi ya Poland.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWINGEREZA ATEULIWA KUCHEZESHA FAINALI YA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top