Kagera,Tanzania.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Majimaji,Danny Mrwanda, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumia Kagera Sugar kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mrwanda aliwahi kuzichezea Simba, Polisi Moro, Yanga katika misimu tofauti kabla ya kusajiliwa na Majimaji katika dirisha dogo la Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Akithibitisha usajili huo,Mratibu wa Kagera Sugar, Mwinyi Mwinyi,amesema wamewasainisha mkataba wa mwaka mmoja Mrwanda na mchezaji mwenzake, Japhet Vedastus kutoka Toto Africans.
Mwinyi alisema usajili huo umetoka na mapendekezo yaliyotolewa na Kocha wao Mkuu,Adolf Richard kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment