728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 08, 2016

    VITAL'O YAITAJIA SIMBA SC BEI YA LAUDIT MAVUGO

    Bujumbura, Burundi.

    KLABU ya Simba imeambiwa iwapo
    inamtaka mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini Burundi, Laudit Mavugo basi ikubali kuzama mfukoni na kutoa
    kitita cha dola za Marekani 100,000 sawa na Sh milioni 200.

    Mwaka jana, klabu hiyo ya Msimbazi ilikurupuka na kumpa dola 10,000 kati ya dola 20,000, ambazo walikubaliana lakini walikwaa kisiki baada ya Vital’O kuwawekea ngumu na kutaka Simba itoe fedha ndefu ili imnase mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Burundi.

    Rais wa Vital’O , Bikolimana
    Benjamin alikaririwa na moja ya radio maarufu za michezo akisema kuwa Simba isijisumbue kwa Mavugo hadi hapo itakapotimiza masharti ambayo wamewapatia ikiwemo kutoa fedha ambazo wamewataka kuzitoa.

    Mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi wana hamu kubwa ya ujio wa Mavugo kauli ya rais wa Vital’O itakuwa mwiba mchungu kwa wana
    Msimbazi hao ambao wana kiu ya ubingwa, ambao wameukosa kwa muda wa miaka minne mfululizo.

    Alisema tangu Simba walipofika nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo ya kunasa mchezaji huyo na kushindwa kufikia makubaliano, hawakurudi tena kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo.

    “Sisi tupo tayari kumwachia Mavugo ajiunge na Simba kwa sababu tuna uhusiano nao mzuri ila tutafanya
    hivyo baada ya kuwa tumemalizana nao.“alisema.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VITAL'O YAITAJIA SIMBA SC BEI YA LAUDIT MAVUGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top