Roma,Italia. Claudio
Marcelo Bielsa amebwaga manyanga kukinoa kikosi cha SS Lazio yakiwa ni masaa 48 tu yamepita tangu atangazwe kuwa kocha mpya wa klabu hiyo ya jiji la Roma.
Juzi Jumatano SS Lazio ilimtangaza,Muargentina Bielsa,60,maarufu kama 'El Loco',(the Madman)/Kichaa kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya aliyekuwa Kocha wake wa muda Simone Inzaghi.
Taarifa zilizoufikia mtandao huu kutoka Italia zinasema Kocha huyo wa zamani wa Argentina,Chile na Mexico pamoja na vilabu vya Espanyol,Marseille na Athletic Bilbao amesitisha mkataba na klabu hiyo leo Ijumaa.
Taarifa zaidi zinasema Bielsa alimpigia simu mmiliki wa klabu hiyo Claudio Lotito Alhamis usiku na kumwambia kuwa hana mpango wa kuendelea na klabu hiyo ambayo ilitarajia kumtambulisha wikendi hii.
Wakati huo huo SS Lazio imetangaza kuwa itamfungulia mashitaka Kocha huyo kutokana na kuvunja mkataba huo.
0 comments:
Post a Comment