Leceister,England.
Leicester City imemsajili Mshambuliaji wa Nigeria,Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa ada ya rekodi ya £16m.
Musa,23,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuwatumikia mabingwa hao wa England na anakuwa mchezaji ghari zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo ya King Power.
Musa anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Leceister City tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya.Wengine ni Ron-Robert Zieler,Luis Hernandez na Nampalys Mendy.
Musa alijiunga na CSKA Moscow mwaka 2012 na mpaka anaiacha klabu hiyo amefanikiwa kuifungia mabao 54 katika michezo 168.
0 comments:
Post a Comment