728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 08, 2016

    MESSI KUPANDA TENA KIZIMBANI HIVI KARIBUNI

    Barcelona, Hispania.

    STAA wa Barcelona na Argentina,Lionel Messi,amesema atapanda tena kizimbani kukata rufaa kupinga adhabu ya kifungo gerezani aliyohukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi.

    Juzi Jumatano Mahakama ya jiji la Barcelona,ilimuhukumu Messi,29, pamoja na Baba yake Mzazi,Jorge Horacio Messi kwenda gerezani miezi 21 pamoja na kulipa faini ya €3.7m baada ya kuwakuta na hatia ya kukwepa kulipa kodi inayokadiriwa kufikia €4.1m.

    Messi kupitia kwa Wanasheria wake Enrique Bacigalupo na Javier Sanchez-Vera,ameripotiwa kuwa anajiandaa kukata rufaa kwa kile kinachodaiwa kuwa adhabu hiyo siyo sahihi akisisitiza kuwa hana hatia.Pia anataka kusafisha jina lake.

    Mapema mwaka jana Messi na baba yake Mzazi,Jorge Horacio Messi ambaye ni wakala wake walidaiwa Kuficha fedha pamoja na kufungua makampuni feki katika nchi za Belize,Uswisi,Uingereza na Uruguay ili kukwepa kodi ya inayotokana mapato ya dili mbalimbali za matangazo alizonazo pamoja na mikataba aliyoingia na makampuni kama vile Danone, Adidas,Pepsi-Cola, Procter & Gamble.

    Bahati nzuri kwa Messi ni kwamba hatatumikia adhabu hiyo kifungoni kwa vile sheria za Hispania zinatoa mwanya kwa watu wenye kifungo cha chini ya miaka miwili na wasio na rekodi ya makosa kutotumikia vifungo vyao gerezani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESSI KUPANDA TENA KIZIMBANI HIVI KARIBUNI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top