Manchester,England.
Vilabu vya Manchester City na FC Barcelona vimefanikiwa kuviimarisha vikosi vyao tayari kwa michuano mbalimbali baada ya leo hii kuwasajili viungo Oleksandr Zinchenko na Denis Suarez.
Manchester City chini ya Kocha Pep Guardiola imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa Ukraine,Oleksandr Zinchenko,toka FC Ufa ya Urusi.
Zinchenko,19,ambaye aliichezea Ukraine michezo mitatu katika fainali za mwaka huu za Euro anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Manchester City tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya.
Akiwa na FC Ufa,Zinchenko,alifanikiwa kucheza michezo 26 akifunga mabao mawili na kupika mengine manne.
Barcelona, Hispania.Barcelona imemsajili aliyekuwa kiungo wake wa zamani Denis Suarez kutoka Villarreal kwa ada ya €3.25m.
Suarez,21,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia miamba hiyo ya Nou Camp wenye kipengele cha kuuzwa kwa €50m.
Akiwa na Villarreal,Suarez, alifanikiwa kufunga mabao matano na kupika 13 katika michezo 48 na kuiwezesha klabu hiyo maarufu kama Nyambizi ya Njano kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.hm
0 comments:
Post a Comment