Hiroshima,Japan.
RASMI Arsenal leo imemtambulisha mbele ya vyombo ya habari mshambuliaji wake mpya raia wa Japan,Takuma Asano "Jaguar",uliyemsajili kutoka klabu ya Sanfrecce Hiroshima inayoshiriki ligi kuu ya Japan maarufu kama J League.
Utambulisho wa Takuma,21,umefanyika mchana wa leo huko Hiroshima Japan na anatarajiwa kujiunga na Arsenal hivi karibuni baada ya kumalizia michezo michache katika klabu yake mama ya Sanfrecce Hiroshima.
Takuma ambaye ameripotiwa kuigharimu Arsenal kitita cha £5m kuipata saini yake anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Japan kujiunga na klabu hiyo ya Emirates.Wengine ni Ryo Miyaichi na Junichi Inamoto.
0 comments:
Post a Comment