Cairo,Misri.
MIAMBA wa Misri,Zamalek wameshindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Petrosport baada ya usiku wa leo kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo mkali wa kundi B wa kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika.
Mabao ya Mamelodi Sundowns yaliyozima shangwe za mashabiki wa Zamalek yamefungwa na Samuel Tiyani Mabunda pamoja na mchezaji bora wa mwaka wa Afrika Kusini,Mzimbabwe Khama Billiat.Mohamed Ibrahim aliifungia Zamalek bao la kufutia machozi.
Matokeo hayo yamewapeleka Mamelodi Sundowns kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kucheza michezo miwili.Zamalek wako nafasi ya pili wakiwa na pointi zao tatu wakiwa wamecheza michezo miwili pia.Nafasi ya mwisho inakaliwa na Enyimba International ambayo haina pointi yoyote imecheza michezo miwili pia.
0 comments:
Post a Comment