Mashabiki wa TP Mazembe
Bejaia,Algeria.
TP Mazembe na Mo Bejaia zimechoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo mkali wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Usiku huu katika Uwanja wa Stade de l'UnitƩ MaghrƩbine,huko Bejaia-Algeria.
Kwa matokeo hayo TP Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A baada ya kufikusanyia pointi saba kufuatia kushuka dimbani mara tatu.Mo Bejaia ni ya pili ikiwa imejikusanyia pointi tano,Medeama FC ni ya tatu ikiwa na pointi mbili huku Yanga SC ikiwa mkiani na pointi yake moja.Timu zote zimecheza michezo mitatu mitatu.
Michezo ya marudiano ya kundi A inatarajiwa kufanyika Julai 27 ambapo TP Mazembe watakuwa wenyeji wa MO BĆ©jaĆÆa huko Stade TP Mazembe,Lubumbashi,Congo DR.Yanga watasafiri mpaka Sekondi-Tokoradi,Ghana kuvaana na Medeama FC
0 comments:
Post a Comment