728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 07, 2016

    HATIMAYE VICTOR VALDES APATA TIMU MPYA ENGLAND

    Middlesborough,England.

    Klabu ya Middlesborough ambayo hivi karibuni imerejea tena Ligi Kuu England baada ya kushuka miaka kadhaa iliyopita leo imemsajili aliyekuwa mlinda mlango wa vilabu vya Manchester United na Barcelona, Muhispania Victor Valdes.

    Valdes,34,amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya jioni ya leo huko Riverside.

    Mkataba huo unaotarajiwa kufikia tamati mwaka 2018 unamfanya Valdes kuwa mchezaji wa tano kujiunga na klabu hiyo.Wengine ni Viktor Fischer, Bernardo Espinosa,Marten de Roon na Jordan McGhee.

    Valdes ambaye alifanikiwa kuichezea Barcelona michezo 535 amejiunga na Middlesborough baada ya kutupiwa virago na Manchester United ambayo alifanikiwa kuichezea michezo miwili pekee kwa kipindi cha mwaka mmoja.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE VICTOR VALDES APATA TIMU MPYA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top