Marseille, Ufaransa.
MABAO mawili ya kila kipindi ya Mshambuliaji, Antoine Griezmann, yameiwezesha Ufaransa kutinga fainali ya Michuano ya Euro baada ya Usiku huu kuifunga Ujerumani kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa katika uwanja wa Stade Velodrome huko Marseille.
Griezmann alifunga bao la kwanza dakika ya 46 kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya nahodha Bastian Schweinsteiger kuunawa mpira ndani ya boksi na mwamuzi Nicola Rizolli kutoka Italia akaamuru ipigwe penati.
Dakika ya 72 Griezmann aliifungia Ufaransa bao la pili baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Ujerumani,Manuel Neuer na kuusukuma mpira langoni.
Ufaransa sasa itavaana na Ureno katika finali siku ya Jumapili Julai 10 huko Saint Denis.
VIKOSI
Germany: Manuel Neuer, Jonas Hector,Jerome Boateng, Benedikt Hoewedes,Joshua Kimmich, Emre Can, Julian Draxler, Toni Kroos, Mesut Ozil,Bastian Schweinsteiger, Thomas Mueller.
France: Hugo Lloris, Bacary Sagna,Samuel Umtiti, Laurent Koscielny,Patrice Evra, Paul Pogba, Blaise Matuidi, Moussa Sissoko, Antoine Griezmann, Dimitri Payet, Olivier Giroud.
0 comments:
Post a Comment