Dar es Salaam,Tanzania.
MKUU wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga,Jerry Muro,amesema mwenye uwezo wa kumwambia akae pembeni ni mwajiri wake ambaye ni Yanga na siyo mtu mwingine.
Muro ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha Michezo kinachorushwa na kituo cha Redio cha TBC Taifa alipotafutwa kuongelea kifungo cha mwaka mmoja alichopewa na TFF jioni ya leo.
Amesema TFF haina uwezo wa kumfungia kwani yeye siyo mwanachama wala mwajiriwa wa shirikisho hilo.
Muro akiongea toka kijijini kwao Machame,mkoani Kilimanjaro,ameongeza kuwa hatambui kufungiwa huko na kusisitiza kuwa kama TFF wanataka kumfungia mtu basi waifungie Yanga kwani ndiyo inayomtuma kusema anachokisema.
Jioni ya leo Kamati ya maadili ya TFF imetangaza kumfungia Murro Kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kumlima faini ya shilingi milioni tatu kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kupingana na maagizo ya shirikisho hilo.
0 comments:
Post a Comment