Newcastle,England.
Klabu ya Newcastle United imeendelea kulitendea haki dirisha la usajili la mwezi januari baada ya leo jioni kumsajili kwa mkopo wa mkopo wa miezi sita mshambuliaji Seydou Doumbia toka klabu ya AS Roma.
Doumbia,28 raia wa Ivory Coast anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Newcastle United katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya Henry Saviet na Jonjo Shelvey.
Kabla ya kusaini Newcastle United Doumbia alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha AS Roma.
0 comments:
Post a Comment