Nairobi,Kenya.
Dirisha la usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Kenya [KPL] limefungwa jana Januari 31 ambapo mabingwa watetezi Gor Mahia [K’Ogalo] wametajwa kuwa klabu iliyotumia pesa nyingi zaidi kusajili msimu huu huku Sofapaka ikisajili wachezaji wapya 25.
Gor Mahia ambayo itaiwakilisha Kenya katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika baadae mwaka huu imetumia jumla ya shilingi za Kenya millioni 4.38 kukiongezea makali kikosi chake.
Kutoka vyanzo vya kuaminika ni kuwa millioni 4 imetumia kumsajili nahodha na Straika wa Rwanda Jacques Tuyisenge ambaye baada ya usajili huo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kusajiliwa kwa pesa nyingi zaidi katika historia ya soka la Kenya.
Pia Gor Mahia imetumia shilingi 200,000 kumsajili mlinzi Luke Ochieng kutoka kCB huku James Ogada akisajiliwa toka Agro Chemicals kwa shilingi 150,000.Edmond Murai, Sammy Okinda, Gradus Ochieng, Eric Otieno na Jackson Saleh wakisajiliwa kwa shilingi 30,000 kila mmoja.
Bandari imetumia shilingi 15,000 kusajili wachezaji watano,AFC Leopard imetumia shilingi 270,000 kusajili wachezaji wapya 21baada ya kuondokewa na wachezaji wake wengi.Batoto Ba Mungu wametumia shilingi 180,000 na Mathare United ikitumia shillingi 30,000.
Ligi kuu ya Kenya inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake wiki ijayo Februari 13.
0 comments:
Post a Comment