728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, October 04, 2015

    KWA HILI ZA AZAM TV, YANGA MMECHEZA KAMA PELE

    Paul Manjale.

    Mapema wiki iliyopita klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wake Yusuf Manji ilitangaza kumaliza mvutano wake wa muda mrefu na kituo Azam TV na kutoa baraka zote kwa kituo hicho kuendelea kuonyesha michezo yake bila matatizo.Mbali ya habari hiyo njema pia Yanga ilitangaza kuwa iko mbioni kuja na kipindi chake cha luninga ambacho kitakuwa kikiruka pia kupitia Azam TV.

    Hii ni habari njema sana kwa mashabiki wa Yanga.Naiita ni habari njema kwani baada ya kumalizika kwa mvutano huo Yanga itavuna mamilioni ya shilingi kama malipo ya michezo yake yote iliyowahi kuonyeshwa kupitia Azam TV.Ikumbukwe Yanga ndiyo timu pekee ya ligi kuu ambayo ilikuwa haijawahi kuonja pesa ya udhamini kutoka Azam TV kutokana na kutoridhishwa na mambo kadha wa kadha lakini kubwa likiwa ni dau la udhamini.

    Binafsi naamini kuwa Kuna faidi nyingi sana ambazo Yanga itazipata baada ya kumaliza mvutano wake na Azam TV.

    Mosi,Kupitia pesa za Azam TV,Yanga itaweza kufanikisha mambo yake mengi ya kimsingi kama vile kulipia gharama za kambi,kulipa posho za wachezaji,kujiwekea akiba kwa ajili ya siku za usoni na mambo mengine mengi ya kimaendeleo ya ndani na nje ya uwanja kubwa likiwa ni kutetea ubingwa wake wa ligi kuu iliyoutwaa msimu uliopita.

    Pili,Kupitia kipindi cha luninga Yanga itapata fursa ya kujiweka karibu zaidi na mashabiki wake.Mashabiki wataweza kupata habari mbalimbali zihusuyo klabu yao kwa mapana na marefu zaidi kuliko ilivyo sasa.Mashabiki pia watapata nafasi ya kujadili kwa pamoja mambo mbalimbali yatakayo kuwa na tija kwa klabu yao.

    Tatu,Kupitia Azam TV,Yanga itapata fursa ya kujitangaza zaidi kimataifa na hii ni kutokana na ukweli kuwa matangazo ya Azam TV kwasasa yanafika karibu kila pande za dunia.Na katika kujitangaza huko Yanga inaweza kujifungulia zaidi milango ya udhamini bila kusahau kuuza wachezaji wake kama vifanyavyo vilabu vingine vya ng'ambo ambavyo hutumia luninga kutafuta masoko kwa ajili ya wachezaji wake.Kilala kheri Yanga,Kilala kheri Azam TV

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KWA HILI ZA AZAM TV, YANGA MMECHEZA KAMA PELE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top