Kama unadhani Arsenal itamwachia kirahisi Alexis Sanchez atimke klabuni hapo pindi klabu yoyote itakapokuwa inamuhitaji,sahau kabisa.
Ziko sababu nyingi sana ambazo Arsenal itazitoa ili tu Alexis Sanchez abakie Emirates,kubwa ni kuwa yeye ndiye injini ya timu kwasasa.
Katika kuthibitisha hilo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ya London zinadai uongozi wa miamba hiyo ya FA unajiadaa kumpa Alexis Sanchez mkataba mpya wa miaka mitano utakaomuwezesha kuvuta mshahara wa £130,000 kwa wiki na mazungumzo rasmi ya mkataba huo yataanza kufanyika katika kipindi cha majira ya sikukuu za Krismasi.
0 comments:
Post a Comment