Licha ya kukiri kuwa yuko katika kipindi kigumu sana cha maisha yake ya ukocha,Jose Mourinho amesema hafikirii kuikimbia Chelsea baada ya kichapo cha goli 3-1 toka kwa Southampton jana jumamosi.
Akiongea baada ya mchezo huo ulioiacha Chelsea katika nafasi ya 13 nyuma ya vinara Manchester City kwa pointi 10,Mourinho amesema
"Matokeo dhidi ya Southampton hayawezi kunifanya nikayakimbia majukumu yangu.Kama Chelsea itaamua kunifukuza,acha inifukuze lakini inapaswa kutambuwa kuwa itakuwa imemfukuza kocha bora zaidi kuwahi kuwa nae"
Wakati huohuo Jose Mourinho ameongeza kuwa kichapo cha jana pia kilichangiwa na makosa ya mwamuzi kwa kukataa kuipa Chelsea penati halali baada ya Radamel Falcao kudondoshwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Southampton.
"Tumenyimwa penati katika mazingira ambayo siyafahamu.Huo ndiyo ukweli.Kama FA itaamua kuniadhibu acha iniadhibu.Haiwaadhibu makocha wengine".
0 comments:
Post a Comment