Wanatuogopa.Hii ni kauli ya kocha wa timu ya taifa ya Wales Chris Coleman kufuatia mataifa ya Hispania,Ujerumani na Italia kudengua kucheza mchezo wa kirafiki na timu yake ili kujiweka sawa kabla ya michuano ya Ulaya (Euro) hapo mwakani nchini Ufaransa.
Coleman amefichua kuwa chama cha soka cha Wales kimekuwa katika mawasiliano ya muda mrefu na mataifa makubwa ya Hispania,Ujerumani na Italia kwa kipindi kirefu sasa lakini mataifa hayo yameonekana kutokuwa tayari kuvaana na kikosi chake na badala yake yamekuwa yakicheza yenyewe kwa yenyewe.
"Nahitaji kukipima kikosi changu dhidi ya mataifa makubwa ili kujua kama kimewiva ama lah lakini hakuna taifa lolote kama ya yale tunayoyataka limeonyesha nia ya kucheza na sisi,inashangaza.Nadhani wanatuogopa kutokana na kiwango kizuri tunachoendelea kukionyesha.Alisema Coleman na kuongeza kuwa wako katika mazungumzo na Argentina ili kucheza mchezo wa kirafiki baada ya Christimasi.
Wales wanaongoza kundi B wakiwa hawajapoteza mchezo wowote huku wakishinda michezo mitano na kutosa sare mara tatu wakitarajia kufuzu michuano ya mwakani tangu walipofanya hivyo mwaka 1958.
0 comments:
Post a Comment