Nyota wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka Paul Merson ametabiri kuwa Crystal Palace itamaliza ligi ikiwa juu ya Liverpool na Tottenham.
Merson ametabiri Crystal Palace itamaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tano na kukata tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.Katika utabiri huo Merson ameitupa Liverpool katika nafasi ya sita, Tottenham katika nafasi ya nane,Manchester City nafasi ya kwanza,Chelsea nafasi ya pili,Arsenal nafasi ya tatu na Manchester United katika nafasi ya nne.
Akitoa majibu ya utabari huo Merson amesema anaipenda Crystal Palace na ikiwa fiti kama timu haitakuwa mbali na nafasi nne za juu.
"Palace haipo katika michuano ya Ulaya na pia ina wachezaji wazuri.Watu wanaweza kusema kuwa Palace haiwezi kuwa juu kwasababu yenyewe siyo Liverpool ama Tottenham lakini ukweli ni kuwa nusu ya wachezaji wa Palace wana uwezo wa kupata nafasi katika vikosi vya kwanza vya Tottenham na Liverpool.Alimalia Merson.
0 comments:
Post a Comment