728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 04, 2015

    BENCHI NOMA!!DEBUCHY ILIBAKI KIDOGO TU NIIHAME ARSENAL

    London,England.

    Mlinzi wa kulia wa Arsenal Mfaransa Mathieu Debuchy ametanabaisha kuwa alifikiria kuihama klabu hiyo katika dirisha lililopita la usajili barani Ulaya.

    Debuchy,30 ambaye alijiunga na Arsenal msimu uliopita akitokea Newcastle kwa ada ya £12m ameeleza jinsi anavyoumia kukaa benchi akiwa chaguo la pili nyuma ya mlinzi kinda Hector Bellerin,20.

    Akifanya mazungumzo toka nyumbani kwao Ufaransa alikokwenda kuitumikia timu yake ya taifa,Debuchy amesema baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimkabili kwa kipindi kirefu msimu uliopita alitegemea kurejeshwa tena katika kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini hali ikawa ni tofauti kwani Bellerin ameendelea kupangwa katika michezo mbalimbali ukiwemo ule wa ngao ya hisani dhidi ya Chelsea.

    "Sikujisikia vizuri Wenger alipompanga Bellerin katika mchezo ule na mimi kuniacha benchi.Niliumia sana na kufikia hatua ya kufikiria kuhama na kwenda kwingineko ambako ningepata muda mwingi wa kucheza ili nijihakikishie nafasi ya kuwemo katika kikosi cha Ufaransa kitakachocheza michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016).



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BENCHI NOMA!!DEBUCHY ILIBAKI KIDOGO TU NIIHAME ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top