Timu za Ligi Kuu Bara zilikabidhiwa jezi na vifaa kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Vodacom, juzi lakini imebainika kuwa Azam FC haitavitumia.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema timu yake imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka kadhaa.
Ingawa hakutoa sababu za kina juu ya maamuzi yao hayo lakini alifunguka hivi:
“Huwa hatuzitumii hizo jezi, msimu wa pili sasa tunatumia jezi zetu wenyewe, cha msingi ni kufuata utaratibu unavyotakiwa kama vile kuwepo kwa nembo ya mdhamini kwenye sehemu husika jezi na mambo mengine, ndiyo maana tunatumia za kwetu wenyewe na hakuna tatizo.
“Zile jezi tunazopewa na mdhamini mara kadhaa huwa tunazigawa kwa timu zetu za vijana au kwingine, hata zile za mazoezi kama bips tunazopewa pia hatuzitumii, tunatumia tunazotengeneza wenyewe na ni kwa sababu tunapenda zaidi kutumia vya kwetu wenyewe.”
0 comments:
Post a Comment