Roma,Italia.
Kadi hizo zitatolewa kwa mchezaji ambaye atafanya yafuatayo kuonyesha mchezo wa kiungwana (fair play),kutoa mpira nje ya uwanja aonapo mchezaji wa timu pinzani ameumia na kuhitaji huduma za kitabibu,mchezaji kumsaidia mwamuzi kuwatuliza wachezaji wenzie pindi mwamuzi anapokuwa amejichanganya kati maamuzi na kumrekebisha.
Taarifa zinazidi kubainisha kuwa wachezaji watakaoonyeshwa kadi hiyo wataorodheshwa na kutambuliwa kwa mchango wao mwishoni wa msimu wa ligi ya Seria B.
Tumezoea kuona kadi za njano na nyekundu katika viwanja vya soka lakini safari hii Waitaliano wameamua kuja na kadi ya kijani.Kutoka Italia habari zinasema ligi ya Seria B ya nchini humo itaanza kutumia kadi hizo wikendi hii.
Kadi hizo hazitahusiana na makosa yasiyo ya kiungwana michezoni kama rafu au mambo mengine yasiyo ya kimichezo bali zitakuwa ni kama zawadi kwa wachezaji ambao wataonyesha vitendo vya kiungwana wakati wote wa mchezo.
Kadi hizo zitatolewa kwa mchezaji ambaye atafanya yafuatayo kuonyesha mchezo wa kiungwana (fair play),kutoa mpira nje ya uwanja aonapo mchezaji wa timu pinzani ameumia na kuhitaji huduma za kitabibu,mchezaji kumsaidia mwamuzi kuwatuliza wachezaji wenzie pindi mwamuzi anapokuwa amejichanganya kati maamuzi na kumrekebisha.
Taarifa zinazidi kubainisha kuwa wachezaji watakaoonyeshwa kadi hiyo wataorodheshwa na kutambuliwa kwa mchango wao mwishoni wa msimu wa ligi ya Seria B.
0 comments:
Post a Comment