Djilobodji:Chelsea imemsajili mlinzi wa kati wa Nantes ya Ufaransa Papy Djilobodji kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 2.7.Djilobodjia,27 raia wa Senegal amesaini mkataba wa miaka minne wa kuwatumikia mabingwa hao wa England.
Jelavic:West Ham imemsajili mshambuliaji wa Hull City Nikica Jelavic kwa kitita cha paundi milioni 3.Jelavic,30 amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo pia utakuwa na nafasi ya kuurefusha zaidi hapo baadae.
Moses:West Ham imeendelea kutumia pesa baada ya kufanikiwa kumsajili kwa mkopo winga wa Chelsea Mnigeria Victor Moses,24.
Telles:Inter Milan imemsajili kwa mkopo wa msimu mmoja mlinzi wa kushoto wa Galatasaray Mbrazil Alex Telles.Inter imefanikisha dili hilo baada ya kutoa €1.3m.
Mori:Everton imemsajili mlinzi Ramiro Funes Mori toka River Plate ya Argentina kwa ada ya paundi milioni 9.5.Mori,24 amesaini miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment