728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 14, 2015

    USAJILI:ADAMA TRAORE ATUA ASTON VILLA AKITOKEA FC BARCELONA KWA MASHARTI KIBAO

    Adama Traoré,19amejiunga na klabu ya Aston Villa akitokea klabu ya FC Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7.Traore mzaliwa wa Mali alikuwa ni miongoni mwa makinda waliokuwa wakitabiriwa kuja kuibeba FC Barcelona siku za usoni lakini kutokana na klabu hiyo kusheheni nyota wakali Villa na Barcelona vimekubaliana kuuziana nyota huyo anayecheza wingi ya kulia.

    Barcelona imeiwekea Villa masharti yafuatayo....
    FC Barcelona itakuwa na haki ya kumsajili Traore muda wowote itakapomuhitaji hii ikiwa kama atafanya vizuri England pia Villa haitaruhusiwa kumuuza nyota huyo kabla ya kuitaarifu kwanza FC Barcelona.

    Traore anatarajiwa kutambulishwa leo usiku wakati klabu yake mpya ya Aston Villa itakapokuwa ikivaana na Manchester United katika mchezo wa ligi kuu.








     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:ADAMA TRAORE ATUA ASTON VILLA AKITOKEA FC BARCELONA KWA MASHARTI KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top