728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 12, 2015

    SARE DHIDI YA SWANSEA YAZIDI KUIKOROGA CHELSEA,MOURINHO AMTOA KAFARA MREMBO EVA CARNEIRO


    Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amemtoa kafara daktari wa timu hiyo, Eva Carneiro, akidai kwamba alichangia kwenda kwao sare 2-2 na Swansea wikiendi iliyopita, ambapo amemwondosha kwenye benchi lake.

    Japokuwa Mourinho alionesha wazi kukasirishwa na hatua ya Carneiro kwenda kumtibu Eden Hazard kwa kitambo wakati Chelsea wakiwa tayari wamempoteza kwa kadi nyekundu kipa wa Thibaut Courtois, ukweli ni kwamba daktari huyo aliitwa uwanjani na mwamuzi Michael Oliver.
     Carneiro and Mourinho exchange words on the touchline during Chelsea's draw with Swansea City
    Mourinho amemshusha cheo daktari huyo mwenye mvuto miongoni mwa washabiki wa Chelsea lakini sasa Mourinho ameamua kumvua kazi zake za kuwatibu wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye mechi. Carneiro aliitwa uwanjani mara mbili na mwamuzi Jumamosi hii.

    Jumanne hii, mwanamama huyo ameelezwa kwamba hatakaa tena kwenye benchi la matabibu wa timu hiyo. Hazard alianguka baada ya kukabiliana na mchezaji wa Swansea, Gylfi Sigurdsson.
     Carneiro will now be axed from the Chelsea dugout by Mourinho following the incident where the Blues boss accused his medical team of being naive and leaving his team in a weaker position on the field
    Picha ya video inaonesha wazi mwamuzi akiwaita mara mbili matabibu hao na laiti  Carneiro angetumia kama utetezi huenda angerejeshewa majukumu yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SARE DHIDI YA SWANSEA YAZIDI KUIKOROGA CHELSEA,MOURINHO AMTOA KAFARA MREMBO EVA CARNEIRO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top