728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 13, 2015

    TRA KUENDESHA SEMINA YA KODI KWA VILABU LIGI KUU,DARAJA LA KWANZA

    Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini (TRA) inatarajiwa kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa klabu zilizopo jijini Dar es salaam, siku ya ijumaa tarehe 14 Agosti katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.

    TRA itaendesha semina hiyo kwa klabu zilizopo ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa vilabu hivyo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.

    Kwa kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa vilabu vilivyopo mikoani kwa lengo la viongozi wa vilabu kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.

    Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.

    IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TRA KUENDESHA SEMINA YA KODI KWA VILABU LIGI KUU,DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top