Klabu ya Mpumalanga Black Aces inayochezewa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Kpah Sherman imeuanza vyema msimu wa 2015/16 wa ligi kuu ya Afrika Kusini (Absa Premiership) baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Free State Stars inayochezewa na Tanzania Mrisho Ngassa katika mchezo mkali uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Goble Park,Bethlehem.
Goli pekee la Mpumalanga Black Aces limefungwa kipindi cha kwanza na nyota Bhongolwethu Jayiya dakika ya 24 huku Mrisho Ngassa akidumu uwanjani kwa dakika 64 kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Venter.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo.....
Free State Stars: Diakite, Mashego, Sankara, Shabalala, Thlone, Somaeb, Masehe, Makhaula, Tshabangu (Mohomi 55’), Ngassa (Venter 64’), Ngcobo (Masana 72’)
Mpumalanga Black Aces: Mabokgwane, Kobola, Hendricks, Ngalo, Nonyane, Ngoma, Khuboni (Mashikinya 88’), Tukane (Mosemaedi 67’ [Mtsweni 90+3’]), Matsi, Jayiya, Mbesuma
0 comments:
Post a Comment