Manchester, England.
Ikicheza bila ya mlinda mlango wake David De Gea Klabu ya Manchester United imeuanza vyema msimu mpya wa ligi kuu ya nchi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspur's.
Goli lililoipa ushindi Manchester United lilitokana na kujifunga kwa mlinzi wa Spurs Kyle Walker dakika ya ishirini na mbili ya mchezo akiwa katika harakati za kuokoa shambulizi kali lililofanya na Ashley Young akishirikiana na nahodha Wayne Rooney.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya ligi hiyo msimu kufunguliwa kwa goli la kujifunga.
0 comments:
Post a Comment