728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 11, 2015

    SIRI IMEFICHUKA:KILICHOIFANYA YANGA IWEKE KAMBI MBEYA SASA HADHARANI



    SIRI ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kuweka kambi jijini hapa kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Agosti 22, mwaka huu, imefichuka.


    Imeelezwa kuwa Yanga wameonyesha kuvutiwa na klabu ya Kimondo FC, iliyomkuza kiungo mshambuliaji wao mpya, Geoffrey Mwashiuya na kuamua kuimarisha ‘undugu’ baina yao kwa manufaa ya pande zote mbili.

    Pia, klabu hiyo ya Jangwani imeelezwa kuvutiwa na kipaji cha Mwashiuya, hivyo kuona ni vema ikaweka kambi jijini humu kama sehemu ya kuwashukuru wakazi wa Mbeya kwa kuwazalishia nyota huyo ambaye ametokea kuteka nyoyo za mashabiki wa Wanajangwani hao nchini na kwingineko.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIRI IMEFICHUKA:KILICHOIFANYA YANGA IWEKE KAMBI MBEYA SASA HADHARANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top