728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 12, 2015

    SHAQIRI AANZA KUILIPA STOKE CITY,MASHABIKI WAPAGAWA VIBAYA!!

    Klabu ya Stoke City imeanza kufaidi matunda ya kumsajili nyota Xherdan Shaqiri toka klabu ya Inter Milan baada ya klabu hiyo leo hii kuripotiwa kuvunja rekodi ya mauzo ya jezi,tiketi,skafu na vifaa vingine vya klabu hiyo kongwe zaidi England.

    Shaqiri,23 alijiunga jana jumanne na Stoke City kwa kitita cha £12m ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo katika usajili/ununuzi wa mchezaji mmoja.

    Lakini habari njema toka kwa miamba hiyo maarufu kama [potter] zinadai kuwa baada ya Shaqiri kutua mashabiki wa klabu hiyo walipagawa na kuvamia vituo vya kuuzia tiketi na kununua tiketi kibao za mechi za nyumbani huku jezi,majarida na vitu vingine vikiongeza mauzo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHAQIRI AANZA KUILIPA STOKE CITY,MASHABIKI WAPAGAWA VIBAYA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top