728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 11, 2015

    RAIS WA URUSI AISAIDIA KLABU ENGLAND KUKAMILISHA USAJILI MKUBWA



    Jana jumatatu klabu ya West Bromwich Albion iliandika historia mpya baada ya kutumia kitita cha paundi milioni 12 kumsajili mshambuliaji Solomon Rondon toka klabu ya Zenit ya Urusi.Kitita hicho ni kikubwa sana kuwahi kutumiwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini England,lakini wakati mashabiki wa klabu hiyo wakifurahia usajili huo upande wa pili wanapaswa kumshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuwasaidia kukamilisha usajili huo mkubwa.
     Salomon Rondon signs for West Brom
    Mwezi mmoja uliopita Putin alisaini muswada mpya wa sheria unaovikataza vilabu vya Urusi kuwa na nyota wengi wa kigeni.Urusi imefikia hatua hiyo baada ya kuendelea kuwa katika kiwango cha uchezaji kandanda huku ndiye ikiwa mwenyeji wa kombe la dunia lijalo mwaka 2018.Sheria hiyo imepitishwa ili kulinda viwango na kandanda la nchi hiyo ambayo siku za hivi karibuni imekuwa siyo tishio tena.
    Venezuela's forward Jose Rondon celebrates after scoring against Colombia
    Hivyo kutokana na sheria hiyo mpya klabu ya Zenit haikuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kumuuza nyota wao Solomon Rondon licha ya kwamba nyota huyo alikuwa ni muhimu sana na ndiye aliyeshisha nafsi ya kwanza katika klabu hiyo kwa upachikaji mabao huku akishika nafasi ya pili katika ligi nzima.Sheria hiyo mpya inazuia vilabu kuchezesha nyota sita wa kigeni katika muda wowote ule.

    Akizungumzia hali hiyo kocha mkuu wa Zenit Andre Villas-Boas amesema [Tumeamua kumuachia Rondon aende zake ili kuendana na sheria zilizopo.Inauma sana mfungaji bora wa pili kwenye ligi leo hii hatakiwi Urusi.]
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RAIS WA URUSI AISAIDIA KLABU ENGLAND KUKAMILISHA USAJILI MKUBWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top