Mpira ni mchezo wenye matukio mengi sana ya kufurahisha japo kuna machache ya kuhuzunisha.Picha iliyoko hapo juu imetengenezwa makusudi na mashabiki wa klabu ya New York Redbull kwa ajili ya kuwadhihaki nyota wa klabu pinzani ya New York City Frank Lampard na Andrea Pirlo kwa kuwaita kuwa ni wazee wamekuja katika nyuma ya kupumzikia/kustaafia.Picha inaonyesha Pirlo 36 na Lampard 37 wakiwa na fimbo ya kutembelea katika mikono yao.
Tukio hilo lilitokea jana katika muendelezo wa mechi za ligi kuu nchini Marekani ambapo timu ya New York City ilikubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa wapinzani wao wakubwa New York Redbull katika mchezo uliopachikwa jina la (Big Apple Derby) kwa magoli ya Bradley Wright-Philips na Felipe Martins.
0 comments:
Post a Comment