Klabu ya West Bromwich Albion imeandika historia mpya katika vitabu vyake vya kumbukumbu baada ya leo hii kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari Salomon Rondon kutoka klabu ya Zenit St Petersburg kwa kitita cha paunti milioni 12.
Kitita hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Englang.Kabla ya kumsajili Rondon West Brom haikuwahi kutumia kitita kama hicho katika usajili tangu ilipoanzishwa miaka mingi nyuma.
West Brom imemsajili Rondon kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikimtegemea zaidi kinda Saido Berahino ambaye kwa kipindi kirefu sana amekuwa akiwindwa na klabu ya Tottenham.
Rondon mzaliwa wa Venezuela ameiacha Zenit baada ya msimu uliopita kuifungia magoli 16 na kuibuka mfungaji bora katika ngazi ya klabu akimzidi Hulk.Jumla msimu uliopita Rondon alifunga magoli 28 katika michezo 57

0 comments:
Post a Comment