728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 11, 2015

    MAN CITY YAANZA LIGI KWA KISHINDO YAIBAMIZA WEST BROM TATU,YAYA TOURE IS BACK




    West Brom,England.

    Magoli mawili ya kiungo Yaya Toure na moja la mlinzi Vincent Kompany yameipa Manchester City mwanzo mzuri wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion katika mchezo pekee wa ligi kuu uliopigwa jumatatu usiku katika uwanja wa Hawthorns.

    Toure alifunga goli la kwanza dakika ya 9 akitumia vyema pasi ya Jesus Navas kabla ya kuongeza la pili dakika ya 24 baada ya kugongeana vizuri na Wilfred Bony goli la tatu limefungwa dakika ya 59 na nahodha Vincent Kompany akitumia vyema pasi ya David Silva.

    Huu ni ushindi mkubwa wa kwanza kwa vilabu vya top four baada ya Chelsea kutoka sare ya 2-2 na Swansea City,Manchester United kuifunga Tottenham 1-0 na Arsenal kufungwa 2-0 na Westham.

    Baada ya ushindi huo Manchester City itaivaa Chelsea katika mchezo ujao wa ligi kuu wikendi hii katika dimba la Etihad.


    Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo....

    WBA:
    Myhill 7, Chester 5, Lescott 6, Dawson 5, Fletcher 5, Morrison 5, Gardner 5, Brunt 5, McClean 5 (Yacob, 45; 6), Berahino 7 (McManaman, 80; 6), Lambert 7 (Anichebe, 74; 6).

    MANCHESTER CITY:
    Hart 8, Sagna 7, Kompany 8, Mangala 7, Kolarov 8, Fernandinho 7, Toure 9 (Demichelis, 80; 6), Silva 10, Navas 8, Sterling 7 (Nasri, 74; 6), Bony 8 (Aguero, 63; 6).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN CITY YAANZA LIGI KWA KISHINDO YAIBAMIZA WEST BROM TATU,YAYA TOURE IS BACK Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top