Kiungo mkongwe, Amri Kiemba amejiunga na Stand United ya Shinyanga.
Kiemba pamoja na kiungo wa zamani wa Yanga, Hassan Dilunga wametua Stand United ambayo sasa inadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia.
Msemaji wa Stand United, Deokaji Makomba amesema wachezaji hao, kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
“Kiemba anatarajia kurejea hapa Shinyanga leo kuungana na wenzake kwa ajili ya kwenda Kahama ambako tutaweka kambi.
“Pia Dilunga suala lake limemalizika naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Stand, chama la wana.”
Mara ya mwisho, Kiemba aliichezea Azam FC ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.
0 comments:
Post a Comment