728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 13, 2015

    MALINZI:RUSHWA NI KAMA NGONO,WAHUSIKA KUKIONA CHA MOTO


    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ametoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayegundulika kujihusisha na rushwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara na zote zinazosimamiwa na chombo kuanzia msimu ujao.

    Malinzi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya
    kusaini mkataba mpya wa Ligi Kuu Bara baina yao na kampuni ya simu
    za mkononi ya Vodacom, ukiwa ni wa miaka mitatu utakaofi kia tamati
    mwaka 2018.


    Rais huyo alisema kuna tatizo kubwa la rushwa katika klabu za soka za hapa nchini na wadau wa mchezo huo kwa ujumla, hivyo kuwaonya viongozi wa soka kuanzia wa klabu hadi vyama, waamuzi pamoja na wachezaji kujiepusha na tabia hiyo kwani yeyote atakayekamatwa na kuthibitika kujihusisha na rushwa, atafungiwa maisha kujihusisha na soka.


    “Yeyote atakayebainika kutoa au kupokea rushwa, awe kingozi, mwamuzi au mchezaji, nitamfungia maisha kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi pamoja na kumpeleka mahakamani,” alisema.
    Malinzi aliwataka wadau wa soka nchini wakiwamo waandishi wa habari, kuisaidia TFF kuzuia kwa kuwakamata wale wote watakaobainika kutoa au kuchukua rushwa, kwani jambo hilo hufanyika kwa siri sana akifananisha na ngono.


    “Rushwa ni kama ngono, wote tusaidiane tumkamate hata mtu mmoja awe mfano kwa wengine ili kutokomeza rushwa katika soka,” alisisitiza Malinzi.


    Msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu ambapo jumla ya timu 16 zitakuwa zikitoana jasho kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Yanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MALINZI:RUSHWA NI KAMA NGONO,WAHUSIKA KUKIONA CHA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top