SIMBA imeshusha vifaa vitatu vipya vya kimataifa ambapo kesho huenda wakacheza mechi yao ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya SC Villa ya Uganda katika maadhimisho ya Simba Day yatakayofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni kipa Luis Rideiro ambaye anacheza soka katika timu ya Sporting B ya Ureno ingawa yeye ni raia wa Brazili, straika Kelvin Ngaisenga kutoka Burundi na alikuwa anacheza timu ya AO Bunjumbura.
Luis anatarajia kuingia kesho asubuhi wakati Ngaisenga ameingia mchana wa leo na wote wawili wana nafasi kubwa ya kusajiliwa moja kwa moja baada ya kocha mkuu Dylan Kerr kusisitiza kutafutiwa wachezaji wa aina hiyo.
Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa beki kutoka Mali, Makan Dembele aliyekuwa akikipiga katika timu ya JS Kavyle ya Algeria yeye atatua Jumatatu kwa ajili ya majaribio.
"Kipa na straika kesho watakuwepo katika maadhimisho yetu na huenda watacheza mechi hiyo ya kirafiki, hao wawili wana nafasi kubwa ya kusajiliwa moja kwa moja tunaamini ni wazuri kwani tumefuatilia wasifu wao," alisema Aveva.
0 comments:
Post a Comment