728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 08, 2015

    KEVIN PRINCE BOATENG NAE AFELI VIPIMO,JERAHA ALILOPATA AKIWA KINDA WA MIAKA 16 LAMNYIMA ULAJI



    Lisbon,Ureno.

    Kiungo wa Ghana Kelvin Prince Boateng ameingia katika orodha ndefu ya nyota waliofeli vipimo vya afya katika kukamilisha mchakato wa kuhamia vilabu vipya.

    Boateng,28 ambaye majuzi alifika katika jiji la Lisbon Ureno kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini kuichezea Sporting Lisbon amejikuta akiikosa nafasi hiyo baada ya klabu hiyo kusitisha zoezi hilo kutokana na nyota huyo kugundulika kuwa na jeraha sugu la goli.

     Akiongea jana ijumaa na mtandao wa SIC Noticias mkurugenzi wa mahuano ya kimataifa wa klabu hiyo Augusto Inacio amesema

    "Boateng alikuwa hapa juzi jumatano kufanya vipimo vya afya lakini mambo hayakwenda vizuri.Tumegundua ana jeraha sugu la goti alilolipata wakati akiwa kinda wa miaka 16.Jeraha hilo ndilo ambalo limekuwa likimsumbua katika miaka hii miwili ya karibuni.Oparesheni aliyofanyiwa ndiyo inayompa tabu kwa sasa"Alimaliza Inacio.

    Taarifa hiyo ambayo ni mpya inapingana na ile iliyotoka kabla ambayo ilidai kukwama kwa uhamisho wa nyota huyo kulitokana na kushindwa kufikia makubaliano juu ya haki za picha/sura ya nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Tottenham na Ac Milan.

    Boateng anakuwa mchezaji wa tatu kefeli vipimo vya afya ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili.Alianza Lombard akija Leroy Fer sasa Kevin Prince Boateng.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KEVIN PRINCE BOATENG NAE AFELI VIPIMO,JERAHA ALILOPATA AKIWA KINDA WA MIAKA 16 LAMNYIMA ULAJI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top