I
Mdachi Memphis Depay ameibuka shujaa baada ya kuifungia klabu yake ya Manchester United mabao mawili na kisha kutengeneza moja katika mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford wenyeji Manchester United waliilaza Club Brugge ya Ubelgiji kwa jumla ya bao 3-1.
Brugge ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 8 tu ya mchezo baada kiungo Michael Carrick kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa.Dakika ya 13 Depay aliisawazishia Manchester United bao kabla ya kuongeza jingine dakika ya 43 na kisha kupiga bao dakika ya 90 lililofungwa na Marouane Fellaini.
Fellaini alifunga bao hilo zikiwa zimepita dakika 10 tu baada ya Brugge kupata pigo baada ya mlinzi wake Brandon Mechele kulimwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi Javier Hernandez.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo...
MAN UTD (4-2-3-1):
Romero 6; Darmian 6, Smalling 7, Blind 7, Shaw 6; Carrick 7 (Schweinsteiger 45, 7), Schneiderlin 7; Mata 7, Januzaj 6 (Hernandez 71, 6), Depay 9; Rooney 6 (Fellaini 84).
CLUB BRUGGE (4-1-3-2):
Bruzzese 6; Cools 4, Mechele 6, Duarte 7, De Bock 6; Simons 5 (Claudemir 40, 6); Vormer 7, Vazquez 8 (Vanaken 78, 6), Bolingoli Mbombo 6; Dierckx 7, Diaby 6 (Oulare 55, 6).
MATOKEO MENGINE
Sporting CP 2-1 CSKA
0 comments:
Post a Comment