728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 04, 2015

    BALAA:RONALDO AMPA MENDEZ KISIWA KAMA ZAWADI YA HARUSI

    Staa wa klabu ya Real Madrid Mreno Cristiano Ronaldo amefanya kufuru baada ya kumpa wakala wake bwana Jorge Mendes kisiwa kama zawadi yake ya harusi.

    Kisiwa hicho ambacho mpaka sasa bado hakijapewa jina kiko nchini Ugiriki.Nchi ya Ugiriki imeripotiwa kuanza kuuza baadhi ya visiwa vyake ili kupata fedha kwa ajili ya kuuimarisha uchumi wake ambao umekuwa ukiyumba kwa siku za hivi karibuni.Bei ya kisiwa kimoja nchini Ugiriki inaanzia €3m

    Ronaldo alikuwa mpambe wa Mendes katika harusi hiyo iliyofanyika jumapili iliyopita huko Porto.Mendez amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Sandra Barbossa aliyezaa naye watoto watatu.

    Wageni waliokuwa katika harusi hiyo ni pamoja na Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson,Rais wa Real Madrid Florentino Perez,Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich.

    Kwa mujibu wa tovuti ya ABC ya Hispania Mendes ni mmoja kati ya matajiri wakubwa nchini Ureno ambaye utajiri wake unadhaniwa kuwa na thamani ya €100m.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BALAA:RONALDO AMPA MENDEZ KISIWA KAMA ZAWADI YA HARUSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top