Klabu ya Juventus imepata pigo baada ya kiungo wake mpya Sami Khedira kuripotiwa kuwa atakuwa nnje ya dimba kwa kipindi cha miezi miwili akiuguza majeraha ya misuli aliyoyapata juzi jumamosi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Marseille.
Katika mchezo huo ambao Juventus ilichapwa magoli 2-0,Khedira alicheza kwa dakika 26 tu kabla ya kutolewa uwanjani kwa machela baada ya kupata maumivu ya misuli.
Taarifa zilizotoka katika mtandao wa klabu ya Juventus mchana wa leo zinasema Khedira atakuwa nnje kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa hivyo kuifanya klabu hiyo kufikiria kusajili kiungo mwingine wa kuziba pengo hilo huku kukiwa na habari kuwa kiungo mwingine wa klabu hiyo Kwadwo Asamoah bado hajapona jeraha lake la goti.
0 comments:
Post a Comment