728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 04, 2015

    ARANGUIZ AIKATA MAINI LECEISTER CITY

    Jitihada za klabu ya Leicester City kumsajili kiungo mahiri wa klabu ya Internacional ya Brazil Mchile Charles Aranguiz zinaelekea kugonga mwamba baada ya nyota huyo kutamka waziwazi kuwa hataki kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini England.

    Aranguiz,26 ambaye hivi karibuni aliisaidia nchi yake ya Chile kutwaa taji la Copa America amekuwa akiwindwa na vilabu vingi vya Ulaya huku Leiceister City ikiwa ndiyo klabu pekee iliyowasilisha maombi rasmi ya kutaka kumsajili katika klabu yake ya Internacional.

    Mapema siku ya ijumaa vyombo vya habari vya England viliripoti kuwa Leceister City na Internacional vimekubaliana kuuziana nyota huyo kwa ada ya €15m kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano binafsi kati ya Aranguiz na Leceister City lakini habari za hivi punde zinasema kiungo huyo anapendelea zaidi kujiunga na Bayer Leverkusen ambayo iko tayari kutoa €10m kuliko Leceister City iliyotayari kutoa €15m.

    Akifanya mahojiano na kituo cha luninga cha RBS,Amesema "Sitaki kujiunga na klabu hii [Leceister City].Kwa sasa niko katika mazungumzo na Leverkusen pekee na ningependa kwenda Ujerumani.

    Tayari nina ofa toka Ujerumani [Leverkusen] ambayo kwangu naiona ni nzuri zaidi.Nikijiunga na Leverkusen nina imani itanifikisha mbali na hilo napenda lifahamike pia kwa uongozi wa Internacional.

    Kama uhamisho huo utakwama nitabakia hapa nikiwa mwenye furaha kama ilivyo kwa familia yangu."Alimaliza Aranguiz.

    Kauli hiyo ya Aranguiz inaongeza machungu mengine kwa Leceister City baada ya kutoswa pia na kiungo mkongwe wa AS Napoli Ghokan Inler ambaye naye ada yake ilishakubaliwa na klabu yake lakini mchezaji husika amekataa.









    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARANGUIZ AIKATA MAINI LECEISTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top