728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 06, 2017

    Manchester City yapigwa marufuku ya kusajili wachezaji wapya kwa kipindi cha miaka miwili


    Manchester,England.

    CHAMA cha soka nchini England (FA) kimeifungia Manchester City kutosajili wachezaji wapya kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kubainika kuwa ilifanya ujanja ujanja kwenye usajili wa wachezaji vijana. 

    Manchester City imekumbwa na kifungo hicho baada ya kubainika kuwa ilifanya mawasiliano na familia za wachezaji wawili ambao tayari walikuwa wamesajiliwa na vilabu vingine kwa lengo la kutaka kuwasajili na kuwapeleka kwenye shule yake ya michezo.

    Hii ina maana kwamba Manchester City haitaruhusiwa kusajili wachezaji walio na umri wa chini kati ya miaka 10 na 18 ambao tayari wameshasajiliwa na vilabu vingine vya juu ama timu za madaraja ya chini kwa kipindi cha miezi 18 ijayo.

    Mbali ya kifungo hicho pia Manchester City imetakiwa kulipa faini ya Pauni 300,000 pamoja na kuvilipa fidia vilabu vyote ilivyotaka kuvipoka wachezaji wao. 

    Mwezi Aprili mwaka huu FA ilitengua sajili tatu za zilizofanywa na Manchester City.Sajili hizo ni zile za kiungo wa Everton mwenye miaka 11 na mwingine mwenye miaka 15 kutoka Wolves.

    Manchester City imekuwa klabu ya pili ya ligi kuu England kukumbwa na adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji vijana baada ya hivi karibuni Liverpool nayo kufungiwa miaka miwili kwa kosa hilo hilo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester City yapigwa marufuku ya kusajili wachezaji wapya kwa kipindi cha miaka miwili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top