728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 11, 2017

    Nyange Kaburu Apinga kusimamishwa kwa Abdi Banda


    Mwandishi wetu , Dar es salaam.               


    Suala la Mchezaji wa Simba , Abdi Banda kusimamishwa kucheza Ligi Kuu wakati akisubiri suala lake la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla wakati akiwa hana mpira kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

    -Banda Alifanya kitendo hicho ambacho hakikuonwa na waamuzi katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 2, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu. Pia Kamati ilibaini kuwa Banda alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Maamuzi ya kusimamishwa Abdi Banda imetokana na  Klabu ya Kagera Sugar kuwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote.

    Wakati kamati ya Masaa 72 ikimsimamisha Banda kucheza Uongoz wa Simba umepinga mamuzi ya kamati hiyo Makamu wa Raisi wa Simba Geofrey Nyange Kaburu Amesema suala hilo halikubaliki hata kidogo Kwani maamuzi hayo si sahihi Kwani chombo ambacho kilitakiwa kujadili haikutakiwa kuwa kamati ya Masaa 72.

    Kaburu alisema "kanuni za Soka Kwa tukio la Banda linaweza kukatiwa Rufaa na kwa sababu ni la uwanjani na halikuadhibiwa na mwamuzi bali liliripotiwa na Kamisaa na kuonekana kwenye  Kanda za Video, hivyo waliopaswa kusikiliza ni chombo cha juu zaidi na sio Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (kamati ya masaa 72)"

    Kaburu amepinga maamuzi hayo kwa kuwa Mchezaji wao hakupata nafasi ya kusikilizwa kama ilivyo kwa mujibu wa kanuni na asili ya kosa lenyewe, Amesema “kwa kuwa tunafahamu jambo hili litakwenda katika kamati ya Nidhamu basi kumsimamisha ni kumzuia asicheze ni kama kumuadhibu bila kumsikiliza, hilo ni kinyume na Kanuni'' 

    Pia Kaburu  ameomba Tff kuharakisha kusikiliza shauri la Banda ili kulinda kiwango chake wamemusimamisha wakati michezo Inaendelea Jambo ambalo linaweza kushusha kiwango chake kinachotegemewa na timu yetu ya Simba na timu ya Taifa 

    Pia kaburu amewaambia TFF waache Unafiki Kwani huko nyuma kuna wachezaji wengi ambao wamewahi kufanya kosa kama hilo lakini hawakuadhibiwa kama hivi, mfano mzuri ni kitendo kilichofanywa na Wachezaji wa Yanga, Donald Ngoma Kwa mchezaji wetu Hassan Kessy pia Amis Tambwe Kwa mchezaji wetu Juuko Murshid sisi tuliliripoti makosa hayo yote TFF Kama walivyofanya Kagera sugar lakini mpaka sasa ni zaidi ya miaka miwili kesi hizo hazijawahi kusikilizwa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nyange Kaburu Apinga kusimamishwa kwa Abdi Banda Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top