728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Malinzi:Njooni muone tunavyomchinja Mnyama leo jioni CCM Kirumba

    Mwanza,Tanzania.

    MSEMAJI wa Mbao FC, Chrisant Malinzi amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao leo jioni wa ligi kuu bara kujionea jinsi wanavyomchinja Mnyama,Simba SC pale kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.

    Malinzi amesema
    wamejiandaa vizuri na hawawezi kuiogopa Simba SC kwa jina wala historia yake.Ameongeza kuwa waliutazama mchezo uliopita wa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar na wakabaini mapungufu kadhaa ambayo watayatumia kuondoka na pointi zote tatu kwenye mchezo wa leo.

    “Tumejiandaa vizuri na tutafanya vizuri na kushinda kwani vijana wako tayari na hatuna hofu na suala la wao kuwafunga Simba SC.Mashabiki wetu waje kwa wingi.Tumejiandaa mwezi mzima kwa ajili ya mchezo huu na michezo yetu yote iliyobaki ya ligi kuu bara
    amesema Malinzi.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Malinzi:Njooni muone tunavyomchinja Mnyama leo jioni CCM Kirumba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top