Dar Es Salaam,Tanzania.
UONGOZI wa Simba SC leo kwa kauli moja umekubali kumpa timu Mfanyabiashara maarufu nchini na Shabiki mkubwa wa klabu hiyo Mohammed Dewji "MO" aliyetangaza kutaka kuinunua timu hiyo kwa Shilingi bilioni 20 na kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa timu kutoka ule na kawaida na kuupeleka katika mfumo wa hisa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika mtandao rasmi wa klabu hiyo mchana huu ni kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao kilichofanyika Juzi Jumatatu katika Hotel ya Serena na kuwahusisha viongozi wa Simba SC pamoja na MO.
Mapema mwezi huu Mohammed Dewji alitangaza azma yake ya kutaka kuinunua Simba SC na kisha kuibadili na kuifanya kuwa timu ya mfano Tanzania na Afrika.Moja ya vitu vikubwa alivyoahidi kuifanyia Simba SC ni pamoja na kuitoa katika bejeti ndogo ya sasa ya bilioni 1.2 kwa mwaka na kuifikisha mpaka bilioni 5.5.
Taarifa kamili hii hapa
0 comments:
Post a Comment