728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 17, 2016

    TFF YAMPA BARAKA HASSAN KESSY KUIVAA AZAM FC LEO


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    HASSAN Ramadhan Kessy leo Jumatano atashuka dimbani kuichezea klabu yake ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC licha ya utata wa uhamisho wake kutoka Simba SC kuwa bado haujapatiwa majibu.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kilichokuwa kifanyike jana Jumanne kushindwa kufanyika na sasa kitafanyika Alhamisi ambapo kitatoa majibu ya kesi mbalimbali zinazohusu masuala mazima ya usajili wa wachezaji.

    Kwa mujibu wa Jonas Kiwia ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF imeamuliwa kwamba, wachezaji wote ambao waliombewa leseni na vilabu vyao,wako huru kucheza mechi ya leo Jumatano. 

    Hii ina maana kwamba,Kessy,anaruhusiwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC na kuipunguzia Yanga presha ya kumkosa Juma Abdul anayesumbuliwa na Majeruhi.

    Mchezo wa Ngao ya Jamii utachezwa saa 10:00 jioni ya leo na utarushwa Live na kituo cha luninga cha Agape Television Network (ATN) pekee.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF YAMPA BARAKA HASSAN KESSY KUIVAA AZAM FC LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top